Lugha ya Kiwsahili ni lugha ambayo
historia yake inamjada na mvutano mkubwa kwa wataalam mbambali, Wataalamu ambao
wametafautiana nasa katika mitazamo yao
na maoni yao kuhusu juu ya suala zima la asli na chimbuko la luhga ya
Kiwsahili, na mivutano hiyo imepelekea kuibuka kwa nadhariya mbali mbali
zinazoelezea asili na chimbuko la lugha ya Kiwsahili. Miongoni mwa nadhariya
hizo ipo inayodai kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya Upwa wa Afrika Mashariki.
Kabla ya kujadili nadharia hii kwanza tutaangalia fasili ya Upwa wa Afrika
Mashariki:
Upwa wa Afrika Mashariki ni maeneo ya pwani ya mwambao wa Afrika Mashariki
wenye urefu wa kilomita 1500km kuanzia
pembe ya Afrika(Somalia) hadi kuteremkia Kaskazini mwa Msumbiji pamoja na visiwa vyote vilivyopakana na
mwambao wa Afrika Mashariki. (Shihabuddin & Mnyampala).
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya Upwa wa Afrika Mashariki, wananadhariya
wa nadhariya hii wanadai kuwa lugha ya
Kiswahili asili na chimbuko lake hasa ni
kutoka katika maeneo ya Upwa wa Afrika Mashariki kuanzia Somalia, Kenya,
Tanzania hadi kaskazini ya Msumbiji.
Wananadhariya wa nadhariya hii wameeleza kuwa Kiswahili kimechimbukia
katika maeneo tafauti ya Upwa wa Afrika ya Mashariki kuanzia Mogadishu, Lamu,
Mombasa, Tanga, Dar es salaam, Kilwa, Mofia, Pemba hadi kaskazini ya Msumbiji.
Kwa kuthibitisha dai hili tutafafanua kwa tupitia Ushahidi wa Kijografia,
ushahidi wa Kilughawiya, Ushahidi wa Kihistoria na Ushahidi wa kiutamaduni.
Kwa kuanzia na Ushahidi wa
kijografiya, katika ushahidi huu tutajikita zaidi katika kuangalia ni maeneo yepi hasa duniani, lugha ya
Kiswahili inazungumzwa na kutumiwa kwa sana na wakazi wake, ni wazi kuwa maeneo ambayo
Kiswahili kinazungumzwa na kutumiwa kwa wingi zaidi ni katika maeneo ya
Upwa wa Afrika Mashariki ambapo katika maeneo hayo wakaazi wake hutegemea na kutumia
Kiwsahili kama ni Lugha ya kwanza katika shughuli zao zote. Hivyo ushahidi huu
unatuthibitishia wazi kuwa chimbuko la Kiwsahili ni maeneo ya Upwa wa Afrika
Mashariki, kwani kitu au jambo lolote lile pale kinapoanzia huwa kinapatikana
kwa wingi kuliko zile sehemu kiliposambaa.
Ushahidi wa Kilughawiya, katika
ushahidi huu tutajikita zaidi katika kuangalia Idadi ya wazungumzaji wa lugha
ya Kiswahili, Ufasaha wa lugha na Mfanano wa lahaja mbali mbali zinazopatikana
katika Upwa wa Afrika Mashariki.
Idadi ya
wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni ukweli uliowazi kabisa kwamba idadi
kubwa ya watumiaji na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili duniani inapatikana
katika maeneo ya Upwa wa Afrika ya Mashriki, kwani wenyeji wa maeneo haya
hukitumia Kiswahili kama ni lugha yao ya kwanza na vile vile wenyeji wa maeneo
haya hawana lugha nyengine badala ya Kswahili yaani hawana lugha za kimakabila
hivyo sifa hii imeweza kuwatafautisha wenyeji wa asili wa Upwa wa Afrika
Mashariki na wazungumzaji wa Kiswahili wa maeneo mengine duniani. Hivyo hoja
hii inathibitisha kuwa Kiswahili kimeanzia katika maeneo ya Upwa wa Afrika
Mashariki.
Ufasaha wa
lugha.Wenyeji asili wa Upwa wa Africa Mashariki huzungumza Kiswahili kwa
ufasaha zaidi yaani kwa usahihi kuliko wazungumzaji wa Kiswahili wa maeneo ya
ndani ya bara la Afrika na maeneo mengine duniani. Hivyo hii inatuthibitishiya
kuwa lugha ya Kiswahili kimeazia katika Upwa wa Afrika ya Mashariki.
Mfanano wa lahaja
za mwambao wa Afrika Mashariki. Lahaja mbali mbali zinazopatikana katika
mwambao wa Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa zinafanana katika matamshi na
msamiati, lahaja hizo ni kama vile Kimtangata, Kitikuu, Kivumba, Kihadimu,
Ki-Unguja mjini, Kitumbatu, Kipemba, Kimvita na Chi-miini.
Mfano I: KIVUMBA KI-UNGUJA MJINI
Baka Paka
Beleka Peleka
Bika Pika
Mfano II: KI-UNGUJA KI-AMU
-vunja -vunda
Mchanga mtanga
Chukua tukua
Mfano III: CHI-MIINI KI-MVITA
-aanza -anda
Mapenzi mapendi
Luma lima
Kwa hiyo,
kutokana na mfanano wa lahaja hizo ni
wazi kuwa lugha hizi zinatokana na msingi mmoja na chimbuko lake ni maeneo ya
mwambao wa Afrika ya Mashariki.
Ushahidi wa kihistoriya.Katika
ushahidi huu tutawazungumzia wageni mbali mbali ambao waliowahi kutembelea
maeneo tafauti tafauti ya Upwa wa Afrika katika karne za mwanzo na kuweza kutaja majina ya vitu mbali mbali kwa lugha ambayo iliyokuwa ikizungumzwa na
wenyeji wa mwambao wa Afrika Mashari katika maandishi yao. Miongoni mwa
wanahistoria hao ni:
Ali – Idrisa
(1100 - 1160). Mgeni huyu alitembelea maeneo ya Zanzibar yaani Unguja, katika
maandishi yake alitaja majina ya vitu mbali mbali ambavyo villivyopatikana
katika maeneo ya Zanzibar, mfano; kikombe, mkono wa tembo, muriami na kisukari.
Freeman
Greville. Huyu ni mtaalam wa kihistoriya, katika makala yake ya “Medieval
Evidence for Swahili” amelezea historia ya
miji mbali mbali inayopatikana katika mwambao wa Afrika Mashariki
ukiwemo mji wa Kilwa, katika mji huu alitaja majina ya utani ya Wafalme wa
kipindi hicho, kama vile nguo nyingi, Mkoma watu na Hasha hazimfiki.
Maelezo haya ya wanahistoriya yanaonesha kwamba lugha ya
Kiswahili ilikuweko na wakaazi wa mwabao wakiitumia lugha hiyo tokea karne za
mwanzo hata kabla ya kuja kwa wageni katika Upwa wa Afrika Mashariki, hivyo inathibitisha
wazi kuwa lugha ya Kiswahili ilichimbukia katika maeneo ya Upwa wa Afrika
Mashariki hata kabla ya ujio wa wageni.
Ushahidi wa Kiutamaduni. Katika
ushahidi huu tutazungumzia shughuli za kiushumi katika jamii ya Waswahili. Kuna
maandishi mengi ya Kihistoriya ambayo yameleza kuwa shughuli kuu ya kiuchumi
iliyokuwa ikifanya naWaswahili ni shughuli za uvuvi. Hivyo tunaporudi na
kuziangalia jamii zinazoishi katika Upwa wa Afrika Mashariki tuaona kuwa
wenyeji wa maeneo hayowanajishughulisha zaidi na uvuvi kwa sababu wamezungukwa
na bahari ya Hindi. Kwa hiyo tuaweza kuthubutu kusema kuwa, wenyeji wa Upwa wa
Afrika Mashariki ndio Waswahili na lugha ya Kiswahili asili yake na chimbuko
lake ni maeneo hayo ambayo manayoishi Waswahili.
UDHAIFU WA NADHARIYA
Kwanza, nadhariya hii imeshindwa kuainisha(kutaja) eneo
mahsusi ambapo Kiswahili kimechimbukia au kuanzia ndani ya Upwa wa Afrika
Mashariki.
Vile vile, nadharia hii imekosa mtaalam hata mmoja aliyefanya
utafiti wa kina kwa kutoa vyanzo na ushahidi utakao tumika kuthibitisha dai
hili kuwa Kiswahili ni lugha ya Upwa wa Afrika Mashariki.
UBORA WA
NADHARIYA
Nadharia hii imepelekea watalaam tafauti tafauti kuanza
kufanya tafiti kina juu ya kuchunguza na kuthibitisha hoja mbali mbali
zinazohusiana na historiya ya lugha ya Kiswahili.
Pia nadharia hii imeweza kuonesha ukweli juu ya chimbuko la
lugha ya Kiswahili, kwani hoja zilizotumika kuthibitisha dai hili ni hoja za
kimantiki yaani ni hoja zenye kuingia akilini.
Kwa ujumla,asili na chimbuko la lugha
ya Kiswahili ni maeneo ya Upwa wa Afrika
Mashariki, ingawa kuna udhaifu wa hapa na pale lakini hoja zilizotumika
kuthibitishia nadhariya hii ni hoja za kimantiki na zenye kukubalika kwa mwenye
taaluma yoyoe yule.
No comments:
Post a Comment